About Us (Swahili)

Chuo cha Moshi Institute of Technology yani M.I.T kina toa mafunzo ya Kompyuta, lugha kama Kiingereza, Kifaransa na Kiswahili kwa wageni . Huduma hizi ni kwa vijana wa shule ya Msingi/Sekondari, wafanyakazi na wanaopenda kujiendeleza katika fani zao mbalimbali.
Kuna kozi za wanaoanza mwanzo kabisa kujifunza Kompyuta, kozi za waliobobea katika matumizi ya Kompyuta. Masomo hasa yanayofundishwa ni Kiingereza kwa ajili ya maongezi na kuandika, matumizi ya Kompyuta, Matumizi ya vifaa vya Kompyuta, Somo Kuhusu Mitandao (kuwa gwiji katika matumizi ya “Internet”), Ufundi wa Kompyuta, Mchana na jioni kuna kozi za watu wazimaambao wengi wao wanakuaga ni waajiriwa au waliojiajiri ndio husoma ili kuongeza sifa na ujuzi katika kazi zao. Tofauti na kozi hizo zilizotajwa hapo juu kuna masomo mengine zaidi ya Kompyuta, kozi ya uhazili. Vyuo vyetu viwili cha Moshi na Himo kuna mfumo wa “Internet ” . Kuna Kompyuta 40 ambazo zilitolewa kama Msaada.
Katika ukurasa huu, utapata kuona kozi amabazo zinatolewa zaidi MIT Moshi na Himo. Unaweza kupata maelezo zaidi, Fomu , Kipeperushi na mawasiliano zaidi maelezo zaidi katika ukurasa tofauti
Kozi mbali mbali
Tunatoa mafunzo ya muda mfupi na mrefu katika Teknohama na biashara. Kulingana na matakwa na uwezo maelezo yanaweza badilika, basi tafadhali fanya mawasiliano nasi ili kupata maelezo kamili. Hapa utapata fomu na kipeperushi
Kozi ya Awali Kompyuta
Kozi hii ni kwa ajili ya mtu ambae hajui kabisa kompyuta na yuko tayari kujifunza hasa matumizi ya kompyuta kikamilifu.
Vipengele vya masomo ni:
1. Matumizi makuu ya Kompyuta (ngazi ya awali na cheti)
2. Msingi wa Teknohama na matumizi kiundani zaidi.
3. Kuandaa programu mbalimbali
Vipengele vya Kozi ya Kiingereza:
Kuongea na kuandika Kiingereza ni kitu cha muhimu sana hasa katika enzi hizi za utandawazi na dunia kuwa kijiji. Tunatoa kozi maaalum ya Kiingereza ambayo itakupa uwezo mkubwa wa kujiendeleza na kufanya mawasiliano zaidi hata na wafanyi biashara wenzako. Kuhitimu kozi itakupa motisha wa kujiendeleza zaidi katika kazi zako na maisha kiujumla.
Vipengele vya Kozi ya Uhazili:
Kozi hii ni kwa walengwa ambao wamejiaanda kusoma uhazili kwa undani zaidi na matumizi ya kiofisi na mafunzo ya teknolojia kwa malengo ya kujiajiri au kuajiriwa.
Utapata elimu ya kompyuta, kupangalia maandishi na maneno na programu maalum. Baada ya masomo haya utaandaliwa kwa ajili ya kua na majukumu na jinsi ya kutatua maswala mbali mbali ya kiofisi.
Uhasibu
Ufahamu na uelewa katika maswala ya uhasibu ni muhimu sana katika maisha. Kupata kampuni yako binafsi, kufanya kazi kwako au katika makazi yako. Muda wa miezi 3 tutakufundisha misingi ya uhasibu na programu za kiuhasibu pia. Baada ya masomo yako utaweza kuafanya mahesabu yako mwenyewe kama Kodi, mahesabu ya kibenki, kuhakiki maendeleo ya biashara yako.
Ubunifu yakinifu
Ubunifu mzuri ni muhimu sana karibu katika kila kampuni endapo unataka kuuza bidha, kufikisha ujumbe, kuandaa matangazo . katkia kozi hii utajifunza misingi na kwa undani zaidi matumizi ya ubunifu na programu husika.
Baada ya kozi hii utakua na uwezo wa kutumia programu hizi kazini, kuandaa nakala zako, kufanya mchanganyiko wa rangi, kutumia vipande mbalimabli vya nakala kwa wakati mmoja, kutumia vifaa vya kuweka rangi, na kubadili mitindo.
Teknohama katika mitandao
Tunafundisha wanafunzi aina za kuunganisha mitandao. Kwa mikono-na ufundishaji, wanafunzipia hujifunza wao kwa wao namna tofauti za kutengeneza mitandao, watajifunza kuweka na kufahamu aina mbalimbali za “Server”, kujua lugha na vitendea kazi hutumika kuandaa kumbukumbu na kuhifadhi kumbukumbu husika.
Umeme
Katika kipindi cha kozi ya umeme utajifunza lugha ya ki-elektroniki, miundo na matumizi yake.
Tutafahamu aina za “circuits, siginal za kidigitali na analogia,” na kutumia mifumo ya kidijitali. Misemo kama (counters, timers, diodes, resistors, waveform generators, logic gates) na misemo mingine kwa sasa inaweza kua huifahamu, ila baada ya kumaliza kozi yako utaweza kabisa kuboresha mifumo mikubwa ya ki-elektroniki.
Ufundi wa kompyuta
Kozi hii ni nzuri hasa kwa wasomi ambao wanahitaji kujiajiri au kuajiriwa katika ufundi wa kompyuta, ufundi wa mitandao, ulinzi kwa kutumia kamera, kufunga kompyuta za “server”. Utajifunza yafwatayo:
1. Muhimu (vipuri vya kompyuta, BIOS, operating systems, file systems, kuweka program katika kompyuta).
2. Mfumo wa mitandao (LAN, TCP/IP, vifaa vya kufunga mitandao…)
3. Aina na vifaa vya mfumo mkuu wa “server” (DHCP, DNS, Web server, email servers, file exchange…)
Uandaaji Tovuti
Kuandaa tovuti inayovutia nzuri unahitaji elimu ya kuandaa tovuti, na lugha za ki-programu. Katika kozi hii utajifunza kuhusu HTML, CSS, na PHP pia utajifunza kuhusu SQL. Vile vile utajifunza kwa programu maalum za kuandaa tovuti kama “CMS frameworks”.
Kubobea katika ufundi wa kompyuta
Diploma ya ufundi wa kompyuta (ngazi ya cheti) cheti hiki ndio cheti muhimu katika soko la Teknolojia.
Programu hii ina vipande viwili ambavyo ni (ufundi halisi wa vipuri vya kompyuta) na (operating system).
Kozi hii ipo wazi kabisa kwani inahitaji ufuhamu tu lugha ya kiingereza. Kozi hii muhimu sana na tunaipendekeza ufanye upgrade, kurekebisha, na kutambua matatizo mbali mbali ya kompyuta na kuyatatua. Mfano utajifunza kuhusu:
1. Muongozo wa awali ya kompyuta na mfumo wake.
2. Matengenezo ya kumpyuta na vifaa vyake.
3. Muongozo wa mfumo wa umeme.
4. Kuwa na ujuzi zaidi wa vifaa vya kopmyuta na mfumo wake.